KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira,imekagua mradi wa maji Ngumbo Group uliopo kijiji cha Mbuli kata ya Ngumbo wilaya ya Nyasa mkaoni Ruvuma unaotekelezwa na wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini(RUWASA) na kuridhishwa na utekelezaji wa mradi huo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Jackson Kiswaga,ameipongeza serikali kupitia RUWASA kwa kuendelea kutekeleza miradi ya maji inayolenga kutatua changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi hasa wanaoishi maeneo ya vijijini.
Ameema,serikali inafanya kazi nzuri kumaliza kero ya maji ili kuwaondolea wananchi usumbufu wa kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo ambapo katika mkoa wa Ruvuma serikali kupitia Ruwasa inatekeleza jumla ya miradi 36 yenye thamani ya Sh.bilioni 66.
Kiswaga aliwaeleza wananchi wa kata ya Ngumbo kwamba,lengo la serikali ni kumaliza ujenzi wa mradi huo haraka ili wananchi wapata huduma ya maji na kamati yake itafuatilia fedha zilizobaki ili mkandarasi aweze kukamilisha ujenzi wa mradi huo haraka iwezekanavyo.
Aidha,amewataka wananchi kuhakikisha wanalinda vyanzo vya maji na kutunza mazingira ili miradi inayotekelezwa iweze kudumu kwa muda mrefu na kuleta tija.
“serikali inatumia fedha nyingi kutekeleza miradi hiyo kwa lengo la kusogeza huduma ya maji,hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha anatunza vyanzo vya maji na kuepuka kukata miti ovyo katika maeneo yao”alisema Kiswaga.
Mjumbe wa Kamati hiyo Charles Mwijage,amewataka wanaume wa kata ya Ngumbo ambao ni sehemu ya wanufaika wa mradi huo kujiandaa kuvuta maji kwenye nyumba zao ili kuunga mkono kauli ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kumtua mama ndoo kichwani.
Naibu Waziri wa maji Maryprisca Mahundi alisema,utekelezaji wa mradi huo unaendelea wakati wananchi tayari wameanza kunufaika kupata huduma ya maji kwa baadhi ya maeneo.
Alisema,serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuongeza mtandao wa maji kwenye vijiji ambavyo havijafikiwa na maji ya bomba ambapo amehaidi vijiji vilivyobaki vitapata maji mwishoni mwa mwezi April mwaka huu.
Naibu Waziri Mahundi,amemuagiza meneja wa RUWASA wilaya ya Nyasa Mhandisi Masoud Samila kumsimamia mkandarasi kampuni ya Nipo Africa Engineering Co Ltd inayejenga mradi huo ili afikishe mtandao wa maji kwenye maeneo yote yaliyopangwa kufikishwa huduma hiyo.
Mbunge wa jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya,amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kupeleka fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miradi ya maji katika jimbo la Nyasa.
Meneja wa RUWASA wilaya ya Nyasa Masoud Samila alisema, mradi wa maji Ngumbo Group awamu ya 11 ulianza kutekelezwa mwezi Novemba 2023 na unatarajia kukamilika mwezi April 2024 na gharama za mradi huo ni Sh.bilioni 2,030,668,500.00.
Samila alisema,fedha hizo zinatoka mfuko wa maji wa Taifa,fedha za serikali kuu na fedha za mpango wa lipa kwa matokeo(P4R) na muda wa utekelezaji wa mradi ni siku 180.
Aitaja faida za mradi huo pindi utakapokamilika ni ni pamoja na wananchi wa vijiji vitano vya kata ya Ngumbo na Liwundi kupata huduma yam aji safi na salama kwenye maeneo yao.
Kwa mujibu wa Samila,faida nyingine ni wananchi wa kata hizo kupata muda mwingi wa kufanya shughuli za kujiongezea kipato na kupunguza magonjwa yatokanayo na matumizi yam aji machafu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.