Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa ameipongeza Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kuandaa kikao kazi muhimu cha siku mbili kilichowakutanisha Maafisa Habari wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoka mikoa yote nchini, kilichofanyika katika Ukumbi wa Jiji la Dodoma, Mtumba.
Akizungumza wakati wa kufunga kikao hicho Msigwa amesema kikao hicho ni hatua muhimu katika kuimarisha utoaji wa taarifa sahihi za serikali kwa wananchi, na kwamba Maafisa Habari wanapaswa kuongeza ushirikiano na vyombo vya habari vya maeneo yao ili kufanikisha lengo hilo.
“Kama tulivyokubaliana, ni lazima mshirikiane kwa karibu na waandishi wa habari katika mikoa na wilaya zenu, mtumie vyema vyombo vya habari vya ndani, na msimamie utekelezaji wa maelekezo ya Mheshimiwa Rais Samia kuhusu kuimarisha vitengo vya habari kwa vifaa na rasilimali,” alisema Msigwa.
Mambo mengine ambayo Maafisa Habari wamekubaliana kuyatekeleza ni kutumia mitandao ya kijamii kwa ufanisi ili kuwafikishia wananchi taarifa za sera, mipango na utekelezaji wa miradi ya maendeleo, pamoja na kuongeza maarifa, juhudi na ubunifu katika kazi zao.
Pia wametakiwa kusimamia majukumu yao kwa weledi na kuepuka kutumika kufanya kazi ambazo hazihusiani na taaluma yao ya habari, ili kuimarisha taswira na ufanisi wa Serikali kwa wananchi kupitia mawasiliano ya kimkakati.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.