Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya shilingi milioni 330 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya msingi katika Kata ya Tinginya, Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma.
Shule hiyo, iliyosajiliwa kwa jina la Kawawa, ina jumla ya wanafunzi zaidi ya 500 wanaosoma elimu ya awali na msingi.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Mathias Manja,ameishukuru serikali kwa kujenga shule hiyo, akibainisha kuwa imeimarisha mazingira ya kujifunza kwa wanafunzi na kuboresha mazingira ya kazi kwa walimu.
Shule hiyo ina jumla ya madarasa nane, ambapo saba yanatumika kwa wanafunzi wa shule ya msingi na mawili kwa wanafunzi wa elimu ya awali.
Kwa mujibu wa Mwalimu Manja, shule hiyo imefanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba na imetoa mwanafunzi aliyefanikiwa kujiunga na shule ya vipaji maalum.
Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo, akiwemo Shehira Musa na Shadriki Matuga, wamemshukuru Rais Samia kwa kuwajengea shule bora yenye mazingira rafiki kwa kujifunzia na kupeleka walimu wanaofundisha kwa ufanisi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.