Mgeni rasmi kwenye ufunguzi huo,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed ambaye aliwakilishwa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Gilbert Simiya, ameipongeza serikali kwa kutoa madaktari bingwa na bingwa bobezi wa Dkt.Samia Suluhu Hassan ambao wamefika kutoa huduma za kibingwa mkoani Ruvuma.
Kanali Abbas ametoa rai kwa madaktari hao kufanya kazi yao kwa ufanisi mkubwa kwa kuwa serikali imeboresha upatikanaji wa vifaa tiba na kwamba serikali inaendelea kuboresha huduma za afya mkoani Ruvuma.
“Katika Mkoa wa Ruvuma serikali imetoa shilingi bilioni 18.721 kutekeleza miradi ya afya ikiwemo ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa,ujenzi wa hospitali za Halmashauri,vituo vya afya na zahanati’’,alisisitiza Kanali Abbas.
Ameitaja miradi mingine iliyotekelezwa mkoani Ruvuma ni ukarabati wa hospitali kongwe ya Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru,Mbinga Mji na ujenzi wa majengo ya huduma za dharura (EMD) katika hospitali za Tunduru,Nyasa,Madaba na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.
Ukarabati wa hospitali kongwe ya wilaya ya Tunduru ambapo seriikali imetumia zaidi ya shilingi milioni 900 kutekeleza mradi huo
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.