Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amewataka Wazazi na Walezi mkoani Ruvuma kuwajibika katika kusimamia makuzi na malezi ya Watoto ili kuijenga jamii bora ya baadae
Akizungumza kwenye uzinduzi wa program jumuishi ya taifa ya malezi makuzi na maendeleo ya mtoto (PJT-MMMAM) Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe, Aziza Mangosongo ambapo hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea
Amesema kuwa lengo kuu la program ni kukumbushana kuwekeza katika malezi ya watoto wenye umri wa miaka 0 hadi 8 kwani ndio umri ambao ukuwaji na ujifunzaji wa mtoto unakua kwa kasi zaidi
“Katika kutekeleza program hii kwenye Wilaya pamoja na Halmashauri tunapaswa kuangalia changamoto zinazotukabili kwa kuishilikisha jamii kwani ukiitazama program watekelezaji wakuu ni wazazi na walezi wanatakiwa kutenga muda wa kukaa na kuwasikiliza watoto ili kubaini changamoto zao ”
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.