Shirika la BRITEN ambalo linajihusisha na utoaji wa elimu ya kilimo kuhusu Pembejeo na mbegu bora limetoa elimu ya matumizi bora ya viuatilifu kwa wakulima wa Halmashauri ya Madaba Wilayani Songea mkoani Ruvuma.
BRITEN imetoa elimu hiyo kupitia mashamba darasa ya mazao mbalimbali ikiwemo zao la mahindi na maharage.
Akizungumza katika mkutano Afisa Kilimo wa BRITEN Elly Nyava amewashauri wakulima wa Mkoa wa Ruvuma kutokata tamaa katika kilimo badala yake wajikite Zaidi katika Uzalishaji wa kilimo chenye tija.
Nyava amewashauri wakulima wa Mkoa wa Ruvuma kuendelea kutumia majukawaa mbalimbali yanayotoa elimu ya kilimo Pamoja na kufuata ushauri wa mabwana shamba na wataalamu wa kilimo ili kuongeza uzalishaji.
Kwa upande wake Kiongozi Ufuatiliaji wa Miradi Rehema Selemani ameitaja faida ya matumizi sahihi ya Mizani ya kidigitali inavyomwezesha mkulima kujua Ujazo wa mazao yake baada ya kuuza mazao hayo
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.