Mkuu wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma amekabidhi vitabu vya kiada kwa wakuu wa shule za msingi 164 vyenye thamani ya shilingi milioni 22.
DC Mangosongo amekabidhi vitabu hivyo na taulo kwa ajili ya wanafunzi wa Kike katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa sekondari ya Kigonsera.
Akizungumza baada ya kukabidhi hivyo hivyo Mangosongo amesisitiza vifaa hivyo vikatumike kwa malengo yaliyokusudiwa na sio vinginevyo..
“Kwa niaba ya wananchi wa Mbinga namshukuru Mheshimiwa Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za kuboresha miundombinu ya vyoo, madarasa na madawati na sasa vitabu lengo kubwa ni kuimarisha na kuweka mazingira wezeshi ya kujifunzia na kufundishia kwa walimu na wanafunzi ili kuongeza ufaulu”,alisisitiza.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Andrew Mbunda amesema Halmashauri ya Wilaya Mbinga imepokea vitabu vya kiada na ziada kwa ajili ya shule za msingi 164 kwa ajili ya darasa la awali, la kwanza,pili na tatu pamoja na taulo za kike kwa watoto ambao wameanza balehe.
Kwa upande wake Mwalimu Agnes Mpika amesema vitabu hivyo vitaongeza ufanisi kwa wanafunzi katika tendo la kujifunza ili kuongeza ufaulu na kukuza ubora wa elimu inayotolewa shuleni.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.