• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

CHUMBA cha amani kilichombeba Papa Leo XIV kipo Mahanje Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: May 22nd, 2025

Na Albano Midelo

Katika kijiji kidogo chenye utulivu wa kimungu kilichopo Mahanje,Halmashauri ya Madaba  Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, kuna chumba cha kawaida – lakini historia yake si ya kawaida hata kidogo.

Ndani ya chumba hiki, miaka 22 iliyopita, alilala mtu ambaye  hivi sasa ni Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani – Papa Leo XIV.

Wakati huo hakuwa Papa. Alikuwa Mtawa na Mkuu wa Shirika la Watawa wa Agustino Duniani, akizuru Tanzania katika ziara ya kichungaji. Ilikuwa mwezi Agosti 2003 alipofika Parokia ya Mahanje, ambako alikaa kwa siku nne, na kulala katika chumba hicho kwa siku tatu mfululizo – akiwa pamoja na watawa wenzake wa Shirika hilo.

Kwa macho ya kawaida, ni kitanda cha kawaida, chumba chenye samani zisizong’ara – lakini kwa walio waamini, kwa walio na jicho la imani, hiyo ni alama ya baraka, historia na heshima kubwa kwa Parokia ya Mahanje na Tanzania kwa ujumla.

Papa Leo XIV alikuwepo hapa – kwa miguu yake mwenyewe

“Alipofika hapa, alikaa nasi kama mtawa mnyenyekevu, hakujionesha mtu mkubwa, lakini alikuwa na utulivu wa ajabu na busara ya kiroho iliyovutia wengi,” anasimulia Padre Titus Raphael Kuyela wa Shirika la Mtakatifu Agustino Tanzania, ambaye ni Paroko wa Parokia ya Mahanje.

“Baada ya kuwasili Mahanje, alikaa nasi, akala nasi, akaomba nasi. Siku iliyofuata alikwenda Jimboni kumtembelea Askofu Mtega – aliyekuwa Baba Askofu wa Jimbo la Songea wakati huo. Lakini akarudi tena hapa, na kulala siku tatu katika chumba hiki. Sasa hiki ndicho tunakiita chumba cha Papa.”

Kutoka Mahanje hadi Vatican: Safari ya Imani

Hakuna aliyedhani, wala kutarajia, kuwa Mtawa huyo kutoka Marekani angewahi kuwa Baba Mtakatifu wa Kanisa la Kiroma. Lakini historia ikaandika jina lake – na Parokia ya Mahanje ikapata nafasi ya kipekee katika ramani ya historia ya kanisa duniani.

“Tuliposikia ametangazwa kuwa Papa nilishindwa kujizuia. Niliruka kwa furaha, nikamwamsha mwenzangu usiku nikamwambia, ‘Njoo uone, mkuu wetu wa zamani wa shirika amechaguliwa kuwa Papa!’” anasema Padre Kuyela kwa bashasha.

Baada ya kuchaguliwa kuwa Papa, picha zake zilianza kusambaa, baadhi zikiwa ni zile alizopiga akiwa hapa Tanzania – ikiwemo Parokia ya Mahanje na kituo cha Wino Madaba, ambako pia aliwatembelea watawa wa Shirika lake.

Mahanje: Parokia yenye historia ya miaka 100

Parokia ya Mahanje iliyoanzishwa mwaka 1926, mwaka huu wa 2025 inatimiza karne moja ya uwepo wa Ukristo katika eneo hilo. Na sasa, historia yake inajipambanua kwa uzito zaidi – kuwa sehemu ya maisha ya Papa aliye hai.

Hili ni tukio la kiimani, kihistoria, na la kipekee ambalo linapaswa kuwekwa katika kumbukumbu za Kanisa na Taifa. Wengi sasa watafanya hija kwenda kuona kitanda cha Papa – wakiamini kuwa ni eneo la baraka na sala.

Baraka kwa Ruvuma, Baraka kwa Tanzania

Ujio wa Papa Leo XIV kabla ya kuchaguliwa kuwa kiongozi wa juu wa kanisa ni ishara ya heshima ya kiroho kwa nchi yetu. Na kwa watu wa Mahanje, ni tukio linalofungua ukurasa mpya wa imani, historia na utalii wa kidini.

“Ni fahari yetu. Hatukutarajia. Lakini Mungu aliamua kuweka alama yake hapa. Tuko tayari kulinda kumbukumbu hii kwa vizazi vijavyo,” anasema Padre Kuyela.

Katika wakati ambapo dunia inatafuta alama za tumaini, chumba hiki – na hadithi hii – vinaendelea kuwatia moyo wengi. Kwa wakazi wa Mahanje, na kwa Wakatoliki kote duniani, kitanda hiki sasa si cha kawaida tena – ni sehemu ya historia ya Kanisa Katoliki duniani.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RUVUMA yaandika historia,Bilioni 45.3 zilivyobadilisha muonekano katika sekta ya afya

    May 27, 2025
  • NDOTO za wasichana zilivyofufuliwa katika sekondari ya Dkt.Samia Namtumbo

    May 27, 2025
  • MADAKTARI bingwa kutoa huduma bobezi kwa gharama nafuu Ruvuma

    May 26, 2025
  • MADAKTARI Bingwa wa Samia waweka kambi ya siku sita Ruvuma

    May 26, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.