Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Mheshimiwa Simon Kemori Chacha, amewataka wafanyabiashara wa madini ya vito wilayani humo kufanyakazi katika eneo moja la biashara lililotengwa.
Agizo hili limetolewa katika kikao kilichofanyika na wafanyabiashara hao kwenye eneo linalojengwa soko la kimataifa la madini ya vito wilayani Tunduru.
Mheshimiwa Chacha amesisitiza umuhimu wa ushirikiano miongoni mwa wafanyabiashara hao ili kukuza sekta ya madini ya vito.
Amewataka wafanyabiasha hao kufanya kazi pamoja katika eneo lililotengwa ambalo litakuwa rahisi kusimamiwa na serikali.
“Tunatambua umuhimu wenu katika kukuza uchumi hususani katika Wilaya yetu ,tunaamua kuboresha miundombinu ili kukuza sekta ya madini”. alisema Chacha.
Mheshimiwa Chacha, ametoa wito kwa wadau kuunga mkono mradi huu muhimu kwa ya ajili ya maendeleo ya wilaya ya Tunduru na Taifa kwaujumla.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Chiza Marando amesema ,ujenzi wa soko la kimataifa la madini ya vito,unaendelea vizuri ambapo amesema soko hilo litatoa mazingira bora kwa wafanyabiashara hao .
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.