Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Mheshimiwa Simon Kapinga amewataka madiwani wa Halmashauri hiyo kuwahamasisha Wazazi na walezi kuhakikisha Watoto wote wanaostahili wanakwenda shuleni.
Kapinga ameyasema hayo wakati anazungumza kwenye Kikao cha robo ya pili cha Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo kilichofanyika Lundusi mji mdogo wa Peramiho wilayani Songea.
“ kuna wanafunzi wamefaulu masomo yao ya kujiunga na kidato cha kwanza lakini mpaka sasa hawajaripoti mashuleni,madiwani wenzangu tushirikiane na watendaji wa kata,vijiji na wazazi kuhakikisha Watoto wote wanaripoti shuleni”,alisisitiza Kapinga.
Mwenyekiti huyo pia amekemea tabia ya baadhi ya wananchi wenye mashamba kuwatumikisha Watoto kwenye ajira mashambani hali ambayo inaathiri ratiba za masomo yao ambapo ametaka tabia hiyo iachwe mara moja.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Neema Maghembe amesema ofisi yake kupitia Idara za Elimu Msingi na Sekondari inaendelea kusimamia mahudhurio ya wanafunzi wa awali,msingi na sekondari ili kuhakikisha wanafunzi wote walioandikishwa na waliopangiwa kidato cha kwanza wanaripoti kwa asilimia 100.
Amesema hadi kufikia Januari 31 mwaka huu wanafunzi wa awali katika shule za Halmashauri hiyo walikuwa wameripoti kwa asilimia 99,darasa la kwanza asilimia 99 na wanafunzi wa kidato cha kwanza wameripoti kwa asilimia 81.2
Hata hivyo Mkurugenzi huyo amewapongeza watumishi na wataalam wakiwemo wakuu wa divisheni na vitengo katika Halmashauri hiyo, kwa kazi nzuri ambazo wamekuwa wakifanya, huku akisisitiza kuendelea kuchapa kazi kwa tija na ufanisi.
Halmashauri ya wilaya ya Songe ani miongoni mwa Halmashauri nane zinazounda Mkoa wa Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.