CHAMA Kikuu cha Ushirika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma (TAMCU Ltd),kimenunua maghala mawili yenye uwezo wa kuhifadhi zaidi ya tani 5,000 za mazao ya wakulima wanaohudumia na Chama hicho.
Meneja Mkuu wa TAMCU Imani Kalembo alisema hayo jana, kwa wajumbe wa mkutano Mkuu maalum uliofanyika katika ukumbi wa Skya Way Tunduru mjini.
Alisema,kwenye maghala hayo kuna mizani kubwa yenye uwezo wa kupima magari,majengo ya ofisi na huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo vyoo.
Alisema,wamepokea taarifa kutoka kwa kamishina wa ardhi mkoa wa Ruvuma ikithibitisha uhalali wa mmiliki wake na kuongeza kuwa majengo hayo yanaweza kununuliwa kwa bei ya juu Sh.milioni 546,063,378 na bei ya chini Sh.milioni 464,100,000.
Aidha Kalembo alisema,baada ya majadiliano ya muda mrefu muuzaji ambaye ni mmiliki wa maghala hayo amekubali kuuza kwa bei ya Sh.milioni 492,000,000.
Kalembo amewapongeza wanachama wa Tamcu ambao kupitia Mkutano Mkuu maalum,wameridhia kununua maghala hayo ambayo yatakuwa sehemu ya vyanzo vikubwa vya mapato kwa Chama Kikuu.
Mwenyekiti wa TAMCU Mussa Manjaule alisema,malengo ya chama hicho ni kuendelea maghala mengi zaidi kwa ajili ya kuhifadhi mazao ya wanachama ambapo kwa sasa wanalazimika kukodi maghala ya watu binafsi kwa gharama kubwa.
Manjaule alisema,wilaya ya Tunduru kupitia Chama kikuu cha Ushirika(TAMCU Ltd) inafanya vizuri na kupata sifa kutokana na kuendesha shughuli za Ushirika kwa haki na kuwataka viongozi wa vyama vya msingi(Amcos)kusimamia ushirika na kuwasaidia wanachama kuongeza uzalishaji wa mazao.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mheshimiwa Julius Mtatiro,amewapongeza viongozi wa Amcos na Tamcu kwa mipango mizuri ambayo itasaidia kuongeza mapato yatakayowezesha kuimarisha vyama vya Ushirika
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.