Tani 10 za mkaa mbadala utokanao na makaa ya mawezimekabidhiwa kwa shule za Msingi 15 na shule za Sekondari 15 za Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kwa ajili ya kupikia lengo likiwa ni kutekeleza agizo la matumizi ya nishati safi lilitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mkaa huo umekabidhiwa na mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Kisare Makori katika Halfa ya Ugawaji wa Mkaa Mbadala Utokanao na Makaa ya Mawe iliyofanyika katika Shule ya Sekondari ya wasichana Mbinga Julai 11, 2024.
Akikabidhi mkaa huo Mhe. Kisare amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Joseph Kashushura kwa kuchukua hatua katika kutekeleza agizo la Mhe. Rais na kusisitiza kuwa huo ni mfano wa kuigwa na wengine.
Amesema" Nikupongeze Mkurugenzi kwa kweli umefanya jambo kubwa sana na la kuigwa sio tu tumekabidhi lakini umeacha alama kwa shule hizi na kuhamasisha taasisi nyingine zitumie mkaa huu"
Akisoma taarifa katika hafla hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Joseph Kashushura amebainisha kuwa katika kutekeleza agizo la Mhe. Rais la katazo la matumizi ya nishati chafu , Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga imeanza na shule za Sekondari na Msingi ili kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa wakati wa kupika chakula.
"Tani hizi zilizotolewa ni moja ya mkakati wa kuhakikisha Halmashauri yetu inatumia nishati safi na kuacha uharibifu wa mazingira kwakuwa miti mingi inakatwa kwa ajili ya kupata kuni au mkaa wa kupikia" Amebainisha Kashushura
Akizungumza kwa niaba ya walimu wakuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mndeme mwalimu Denterias Mgaya amesema mkaa huu utapunguza gharama lakini pia ni chachu katika kutunza mazingira.
Watengenezaji na wauzaji wa mkaa huo ni kikundi cha wanawake Mbalawala kilichopo kata ya Ruanda kikundi ambacho ni wanufaika wa mkopo wa 10% unaotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.