Wakulima wa korosho Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wamekubali kuuza korosho zao tani 4,017 katika mnada wa pili wa zao hilo.
Mnada huo ulifanyika katika kijiji cha Amani chama cha ushirika cha msingi CHAMANA (CHAMANA AMCOS), kupitia Mfumo wa Stakabadhi ghala, chini ya Chama kikuu cha Ushirika Tunduru TAMCU LTD.
Wananunuzi 18 walionesha nia ya kununua Korosho Tani 4,017 ambazo ziliingia sokoni katika mnada huu wa pili, wanunuzi watano walishinda kununua Korosho hizo zilizopo ghalani kwa bei ya shilingi 1,831 kwa kilo.
Akizungumza baada ya kutangaza bei hiyo ya zao la korosho Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Ushirika TAMCU LTD Ndg. Mussa Manjaule amewasihi wakulima kutotegemea zao moja la kibiashara na kuwataka kulima kilimo cha mazao mchanganyiko, na kuviomba vyama vya msingi kulipa fedha za wakulima kwa wakati.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.