Wakala wa barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Nyasa, katika mwaka wa fedha wa 2021/2022 imetengewa Bajeti ya tsh Bilioni 2.45 kwa ajili ya Matengenezo ya barabara katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa.
Meneja wa Wakala wa barabara za Mijini na Vijijini TARURA, Mhandisi Thomas Kitusi ameliambia jana Baraza la madiwani katika Ukumbi wa Kepten John Komba, Mbamba bay wakati akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa shughuli za uendaji kazi wa wakala hao Wilayani Wilayani hapa.
Mhandisi Kitusi amefafanua kuwa, kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 TARURA Nyasa imetengewa kiasi cha tsh milioni 950 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kutoka mfuko wa barabara na milioni 500 kwa ajili ya maendeleo kupitia Jimbo kutoka Serikali kuu na nyongeza ya bajeti kutoka tozo ya mafuta wamepewa Tsh Bilion moja.
Amezitaja barabara zitakazojengwa ni Ujenzi wa barabara ya Lami kuanzia Bomani hadi Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa,na matengenezo ya barabara ya Luhindo Mpepo Darpori, kwa kuwa ni barabara yenye changamoto kubwa na ni barabara ya mpakani. Amitaja barabara nyingine kwa ni Kingerikiti Lumeme, kikolo hadi Mtipwili ambayo ni barabara fupi ya kutoka Tarafa ya Mpepo kuja Nyasa.
Aidha amesema fedha nyingine ameelekeza maeneo ambayo hayajawahi fikika, Tangu Uhuru kama Njambe kwenda Ndonga, na kutoka Mbaha kwenda Mpopoma ambako hawana mawasiliano ya barabara.
Ametoa wito kwa Madiwani kuanisha barabara za kipaumbele na wainishe mapendekezo ili ziweze kufanyika kazi.
Kwa upande wao Baraza la madiwani limetoa wito kwa Meneja huyo kushirikiana na uongozi wa Kata na Vijiji ili kuweza kuainisha barabara ambazo wanazitumia na wangependa zitengenezwe wakati wa uandaaji wa utekelezaji wa miradi ya barabara kwa kuwa kuna uhitaji mkubwa wa matengenezo ya barabara na madaraja katika kata zote za Wilaya ya Nyasa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.