MICHEZO ya UMISSETA Mkoa wa Ruvuma imefungwa rasmi kwaajili ya kwenda kushiriki kitaifa Mkoani Tabora.
Michezo hiyo imefanyika katika Chuo cha Ualimu Songea na imefungwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Steven Ndaki .
Ndaki amewapongeza kwa kufikia hatua ya mashindano na kupata fursa ya kushiri kitaifa Mkoani Tabora kuanzia Agosti 8,2022 watakuwa wanasafiri.
“Mlianza Ngazi ya Madarasa pale Shuleni mkafika Shule kwa Shule Kata,Wilaya na Halmashauri hadi Mkoa kwa kweli mmeonyesha juhudi sana”.
Ndaki ametoa rai kwa Viongozi kuwa vitu vizuri vinagharama na bila kufanya hivyo matunda hayawezi kupatikana.
“Mnatakiwa kujua mchezaji bora hutumia fedha nyingi sana katika kuandaa maandalizi kwa mantiki hiyo siyo lelemama hatuwezi kukwepa gharama”.
Amesema kwa kuwa tunatarajia vijana kurudi na ushindi lazima viongozi mmpambane kuwaandaa vizuri na mwisho wa mashindano hayo ni mwanzo wa mashindano mengine.
Afisa Michezo wa Mkoa wa Ruvuma Antony Luoga akisoma taarifa kwa mgeni rasmi amesema mashinda ya Umisseta nyanakuja baada ya Umitashumta kufanyika ambayo yalianza Julai 17 hadi 27 Julai ikiwa wanafunzi 120 na Viongozi 20 waliwakilisha Mkoa katika Mashindano ya Taifa Tabora.
“Tupo kuandaa Timu nyingine ya UMISSETA ambayo Agosti 8,2022 Jumla ya wanamishezo 120 na Viongozi 17 watasafiri kuelekea Tabora”.
Afisa Michezo amesema mashindano ya Mwaka huu katika ngazi ya Mkoa imeanzishwa katika taaluma ambapo kila shule katika Halmashauri imetakiwa kuleta wanafunzi Mahili katika masomo ya Hisabati,Kingereza, Kiswahili kwa kidato cha pili cha tatu na kidato cha Nne ili kuongeza Hamasa katika Taaluma kwa Vijana.
Kufuatia Mashindano hayo amesema kwa mwaka huu 2022 Kitaaluma Wilaya ya Tunduru imeongoza na kuchua nafasi ya Kwanza Kimkoa.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Serikalni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Agosti 4,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.