MKUU wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge,ameipongeza Halmashsuri ya wilaya ya Tunduru, kwa kusimamia vizuri mapato na matumizi ya fedha za Serikali na kuiwezesha kupata hati safi katika mwaka wa fedha 2020/2021.
Brigedia Jenereli Ibuge,ametoa pongezi hizo jana wakati akizungumza na Madiwani na watumishi wa Halmashauri hiyo katika kikao maalum cha Baraza la madiwani cha kujadili taarifa za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kilicho fanyika kwenye ukumbi wa Klasta ya Walimu mjini Tunduru.
Alisema,Halmashauri ya Tunduru imefanikiwa kukusanya jumla ya Sh.bilioni3,263,703,145 sawa na asilimia 106 kati ya lengo la kukusanya Sh.bilioni 3,076,638,496 kwa mwaka fedha 2020/2021.
Rc Ibuge alisema kuwa, mafanikio hayo yametokana na watumishi na madiwani kujisahihisha kwa makosa yaliyofanyika mwaka wa fedha 2020/2021 ambapo Halmashauri hiyo ilipata hati yenye mashaka hali iliyotia doa kwenye rekodi zao za kupata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo.
Ibuge,amewaomba Madiwani na watendaji wa ngazi mbalimbali wa Halmashauri hiyo, kuongeza bidii zaidi katika utendaji wao wa kila siku kwa lengo la kuhakikisha kuwa,hati safi zinaendelea kupatikana kwa kaguzi zijazo.
Amewapongeza madiwani na wadau wengine, kwa kuweza kuchangia kwa asilimia 100 mfuko wa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu ambapo jumla ya Sh.milioni 409,946,884 zimetolewa.
Mkuu wa mkoa alisema, kati ya fedha hizo Sh.163,978,738 zimekwenda kwa vikundi 54 vya wanawake,Sh.163,978,738 kwa vikundi 53 vya vijana na Sh.81,989,369 zimetolewa kwa vikundi 34 kwa watu wenye ulemavu.
Alisema utelekezaji huo umeendana na maelekezo ya serikali ya awamu wa sita inayo sisitiza uwezeshaji wa jamii yote ikiwamo makundi hayo maalumu ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.
Aidha alisema,licha ya kupata hati safi lakini mwenendo wa ushughulikiaji wa Hoja,Mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali pamoja na maagizo ya LAAC katika Halmashauri hiyo unaridhisha kwa kiwango kikubwa.
Kwa mujibu wa Mkuu wa mkoa ni kwamba, wakati wanajadili taarifa ya fedha ya mwaka 2019/ 2020 kulikuwa na hoja 26 ambazo zilikuwa bado hazijafanyiwa kazi pamoja na agizo 1 la LAAC.
Hata hivyo alisema,kati ya hoja hizo 26 za miaka ya nyuma hoja 23 zimehakikiwa na kufungwa,hoja zinazoendelea na utekelezaji ni 3 na agizo 1 la LAAC la miaka ya nyuma limetekelezwa na kufungwa.
Pia alisema, kwa upande wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2021 jumla ya hoja na mapendekezo Ishirini na nane aliyoyatoa CAG yamefanyiwa kazi kati ya hizo kumi na saba yamefungwa baada ya uhakiki.
“huu ni mwenendo mzuri sana ,ninawapongeza kutokana na mnavyoshughulikia hoja na mapendekezo ya CAG katika Halmashauri yenu”alisema Ibuge.
Hata hivyo Balozi Ibuge, akatumia nafasi hiyo kuwaagiza viongozi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanakamilisha utekelezaji wa majibu ya hoja na mapendekezo 14, hoja 3 za miaka ya nyuma na 11 za mwaka wa fedha 2020/2022 kabla ya tarehe 30 Juni mwaka huu.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro alisema,wamepokea viuatilifu vya zao la Korosho kati ya hizo dawa za maji kwa asilimia 90 na upande wa dawa za Unga(Sulpher) wamepokea mifuko elfu 13,000 kati ya mifuko elfu 81 waliyopangiwa .
Akizungumzia hoja za mkaguzi mkuu na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali alisema kuwa, ana uhakika madiwani na wataalamu za Halmashauri hiyo watatekelezaji haraka kujibu hoja na mapendekezo yaliyobaki.
Awali Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Haillu Mussa alisema, Madiwani kwa kushirikiana na wataalamu wa Halmashauri yake wamejipanga kujibu na kutekeleza maagizo na hoja zote ili Halmashauri hiyo iendelee kupata hati safi mwaka hadi mwaka.
Mwisho.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.