Katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma alfajiri ya Aprili 26, wananchi wa Songea, wakiwa wamebeba bendera za Taifa, walikusanyika kwa shangwe kuadhimisha miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tukio liliojaa heshima, uzalendo na mshikamano.
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Mhe. Kapenjama Ndile, aliongoza maadhimisho hayo yaliyopambwa na maandamano ya amani, upandaji miti, na usafi wa mazingira ishara za kudumisha maisha yenye umoja na maendeleo.
Akihutubia umati huo uliokusanyika, Mhe. Ndile alisisitiza dhamira ya Muungano wa Tanzania si zawadi ya bahati, bali ni jitihada za kizalendo za viongozi wetu. Leo hii tunawajibika kulinda tunu hii kwa mshikamano, heshima na kuhimiza amani miongoni mwetu.”
Katika hafla hiyo, alitoa wito maalum kwa watumishi wa umma na wananchi kuwa nguzo za amani, akisisitiza kuwa kila kauli na kila kitendo kinapaswa kuijenga Tanzania moja, yenye mshikamano thabiti.
Simulizi ya historia ya Muungano ilipewa uzito zaidi na Mwenyekiti wa Wazee Wilaya ya Songea, Sofia Namananda, ambaye alikumbusha kwa hisia juhudi za waasisi wa Muungano, Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Amani Karume.
“Muungano Wetu ni Dhamana, Heshima na Tunu ya Taifa — Shiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.”
Kwa Songea na Tanzania nzima, Aprili 26 si tu kumbukumbu ya siku za kale; ni ahadi ya kuendeleza mshikamano, kuilinda dhamira ya waasisi, na kujenga kesho yenye amani zaidi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.