uchomaji misitu hovyo unaofanyika karibu kila mwaka katika Msitu wa Serikali wa Matogoro uliopo katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma hali inayoleta athari za kimazingira kwa kuwa msitu huo ni chanzo cha mito muhimu mitatu mikubwa.
Mito hiyo ni Ruvuma ambao unamwaga maji yake Bahari ya Hindi,Mto Luhira ambao ndiyo chanzo cha mto Ruhuhu unamwaga maji yake Ziwa Nyasa na Mto Luwegu ambao unachangia asilimia 19 ya maji katika Mto Rufiji ambao unaingia Bahari ya Hindi.
Mto Luhira ndiyo chanzo muhimu cha maji ambacho kinategemewa na Mamlaka ya Maji safi na Maji Taka Songea (SOUWASA) kwa ajili ya kusambaza maji katika Mji wa Songea.
Afisa Maliasili wa Mkoa wa Ruvuma Africanus Challe anasema Moto katika msitu wa Matogoro unateketeza eneo kubwa ambapo watumishi wa msitu huo kila mwaka wanafanya jitihada za kukabiliana na athari za uchomaji moto ikiwemo kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya moto kimazingira.
Challe anatoa rai kwa wananchi wanaozunguka msitu huo na kwa wadau wa mazingira wote kushirikiana na hifadhi ya misitu hiyo kukabiliana na matukio ya moto katika milima hiyo ili kuzuia uharibifu wa mazingira unaosababishwa na uchomaji wa moto kwenye msitu huo.
Anasema kutokana na uchomaji moto unaoendelea kufanywa ofisi ya hifadhi ya mlima Matogoro imefanya mazungumzo na mabonde ya maji ya ziwa Nyasa na bonde la maji ka mto Ruvuma ili kusaidiana kupanda miti ya asili katika maeneo yote ambayo yamevunwa miti na yalioungua ambapo mabonde yamechangia katika mradi wa miti.
Anasema Idara yake imechukua hatua mbalimbali za kulinda na kuhifadhi Msitu wa Serikali wa Matogoro na kuzuia uchomaji moto hovyo ambapo mwaka huu hadi sasa hakuna matukio ya moto kwenye msitu huo.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma
Septemba 17,2020
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.