• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

UFUTA waingiza bilioni tatu Tunduru

Imewekwa kuanzia tarehe: June 10th, 2025

Wakulima wa kijiji cha Mcheshi, Tarafa ya Lukumbule, Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wamevuna neema katika mnada wa kwanza wa zao la ufuta msimu huu, ambapo tani 1,273.487 zenye thamani ya Shilingi bilioni 3.1 ziliuzwa kupitia Chama cha Msingi cha Ushirika cha Mruji Amcos.

Meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika Tunduru (TAMCU), Marcelino Mrope, alisema bei ya chini ilikuwa Shilingi 2,410 kwa kilo, ya juu Shilingi 2,460, huku wastani ukiwa Shilingi 2,439—bei ambayo ni pungufu kidogo ikilinganishwa na msimu uliopita.

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mheshimiwa Simon Chacha, alieleza kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya mazingira bora ya soko yaliyowekwa na Serikali kupitia Wizara ya Kilimo.

Amesisitiza kuwa mfumo wa stakabadhi ghalani utaendelea kuimarishwa ili kuwahakikishia wakulima masoko ya uhakika na bei nzuri.

Alitoa wito kwa wakulima kutumia taasisi za kifedha kupokea malipo yao badala ya kubeba fedha taslimu, huku akiwahimiza kutumia mapato kuboresha maisha yao badala ya kuzitumia kwa anasa.

Kwa upande wake, Kaimu Afisa Kilimo wa Wilaya ya Tunduru, Gallus Makwisa, alieleza kuwa wakulima wa Tunduru wamevuka lengo kwa mara ya pili mfululizo kwa kuzalisha tani 8,000 mwaka 2024 kutoka tani 4,000 mwaka 2023.

Halmashauri kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa wa Ruvuma imesambaza tani 8,000 za mbegu bora katika kata 36, lengo likiwa ni kuongeza tija na ubora wa ufuta unaokidhi ushindani wa soko la ndani na nje ya nchi.

Afisa Masoko wa TAMCU, Stella Msengi, alieleza kuwa msimu wa 2024/2025 umevuka matarajio kwa kukusanya kilo 8,774,621 za ufuta, sawa na ongezeko la asilimia 60.09 ikilinganishwa na msimu uliopita.

Alisema matarajio kwa msimu wa 2025/2026 ni kukusanya kilo 12,811,100, huku akiwahamasisha wakulima kuendelea kushirikiana na vyama vya msingi ili kunufaika na mfumo wa mnada unaowaletea tija kubwa.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WAKULIMA Ruvuma waomba soko la mahindi kufunguliwa haraka

    June 16, 2025
  • SERIKALI ,dini na wananchi Ruvuma waungana kudumisha amani

    June 16, 2025
  • RUVUMA yaandika historia chupa 4040 za damu zakusanywa kuokoa maisha

    June 15, 2025
  • NAMTUMBO yaagizwa kuongeza kasi ya kushughulikia hoja za CAG

    June 15, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.