UTALII wa uwindaji unaofanyika katika Jumuiya ya Hifadhi ya wanyamapori ya Mbarang'andu wilayani Namtumbio mkoani Ruvuma imekuwa kivutio kikubwa cha watalii kutoka nchi za Ulaya na Marekani ambao wanatembelea jumuiya hiyo yenye vijiji saba na kufanya aina hiyo ya utalii ambayo inahusisha moja kwa moja matumizi ya wannyamapori.Jumuiya hiyo inahusisha vijiji saba ambavyo ni Mchomolo,Kitanda,Likuyuseka Maganga,Kilmasela,Nambecha,Songambele na Mtelemwahi.
Afrikanus Challe ni Afisa Maliasili na Utalii wa Mkoa wa Ruvuma ambaye anasema utalii wa uwindaji ambao umekuwa unafanyika katika mapori ya akiba yaliyopo sehemu mbalimbali nchini na kwamba aina hiyo ya utalii inakwenda sanjari na utalii wa picha ambao ni utalii wa kutazama mandhari na kupiga picha bila kuhusisha uwindaji wa wanyama na kwamba utalii wa picha pia husisha matumizi ya moja kwa moja ya wanyamapori.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.