MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme anatoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya miaka mitano kuanzia mwaka 2015 hadi 2020
SEKTA YA ELIMU
Idadi ya Shule; Tangu mwaka 2015 hadi 2020 Mkoa umekuwa na ongezeko la idadi ya shule za msingi 103 kutoka idadi ya shule 670 zilizokuwepo mwaka 2015 hadi shule 773 mwaka 2020. Shule za sekondari zimeongezeka kutoka idadi ya shule 111 mwaka 2015 hadi shule 205 kufikia mwaka 2020 sawa na asilimia 54 ambalo ni ongezeko la shule 94.
Uandikishaji wa wanafunzi umeongezeka na kuimarika ambapo kuna ongezeko la uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza kwa idadi ya wanafunzi 50021 hadi kufikia Juni 2020 ukilinganisha na idadi ya wanafunzi 47978 mwaka 2015 sawa na ongezeko la asilmia 4.2 .
Mafanikio ya uandikishaji na mahudhurio ya wanafunzi yameimarika pia kwa upande wa elimu ya Sekondari ambapo hadi Juni 2020 kuna wanafunzi 74,613 ukilinganisha na wanafunzi 55,643 waliokuwa shuleni mwaka 2015. Ongezeko hili ni la wanafunzi 18,970 sawa na asilimia 75.
Mafanikio haya yametokana na Mpango wa Utoaji wa Elimu Bure unaowezeshwa na Serikali ya awamu ya tano ya Mhe, Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ikiwa ni pamoja na;
Hali ya ufaulu wa mtihani ya Kitaifa; Ufaulu katika mitihani ya darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita umeongezeka hadi mwaka 2019 ukilinganisha na hali ilivyokuwa mwaka 2015.
MWAKA
|
WALIOFAULU
|
ASILIMIA
|
MTIHANI
|
2015
|
17298
|
68.4
|
DARASA LA SABA
|
2019
|
26534
|
83.70
|
|
2015
|
6868
|
74.58
|
KIDATO CHA NNE
|
2019
|
10226
|
86.06
|
|
2015
|
1199
|
81.7
|
KIDATO CHA SITA
|
2019
|
3572
|
99.72
|
Miundombinu katika Sekta ya Elimu;
Katika kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi Mhe, Rais ametupatia fedha za utekelezaji wa miradi ya sekta ya elimu kiasi cha shilingi 15,328,933,835.29 kuwezesha uwepo wa miundombinu katika Sekta ya Elimu kama inavyoonesha katika jedwali lifuatalo;
ELIMU YA MSINGI |
||||
AINA
|
IDADI YA MIRADI |
THAMANI (TSH.) |
||
Ujenzi wa Madarasa mapya
|
461
|
4,495,680,244.17 |
||
Ukamilishaji wa maboma ya vyumba vya madarasa
|
67
|
837,500,000 |
||
Ujenzi wa nyumba za walimu
|
36
|
543,255,117 |
||
Ofisi za walimu
|
24
|
172,032,650 |
||
Jumla ndogo
|
|
6,048,468,011.17 |
||
ELIMU YA SEKONDARI |
||||
AINA
|
2015 -2020
|
|||
Ukarabati wa Shule Kongwe
|
3
|
2,882,868,464.65 |
||
Ujenzi wa vyumba vya madarasa
|
235
|
3,271,798,602.04 |
||
Nyumba za walimu
|
6
|
180,080,500 |
||
Jengo la Utawala
|
1
|
50,000,000 |
||
Matundu ya vyoo vya wanafunzi
|
74
|
194,899,282 |
||
Mabweni
|
14
|
852,827,000 |
||
Ukamilishaji vyumba vya maabara
|
68
|
1,847,991,975.43 |
||
Ujenzi wa mabwalo ya chakula
|
6
|
1.732, 542,833.41 |
||
Viti vya wanafunzi
|
7281
|
161, 786,300 |
||
Meza za wanafunzi
|
6836
|
177, 266, 540 |
||
JUMLA
|
9,280,465,824.12 |
|||
|
|
|
|
|
Mhe. Rais amekuwa akiupatia Mkoa fedha kwa ajili ya kutekeleza Mpango wa Elimu Bila Malipo tangu mwaka 2015 ambapo jumla ya Tshs. 26,707,325,111.30 zimepokelewa kwa muda wa miaka mitano hadi kufikia mwaka 2020.
Tunaendelea kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt.John Pombe Joseph Magufuli kwa kuanzisha Mpango huu wa elimu bure kwa watanzania.
Vituo vya Ufundi Stadi na VETA
Katika utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, Mhe, Rais ameboresha eneo la mafunzo ya ufundi stadi ambapo kwa Mkoa sasa kuna vyuo 3 vya VETA hadi mwaka 2020 kutoka chuo 1 mwaka 2015. Hii ni baada ya kuletewa fedha za ujenzi wa vyuo 2 vya VETA vya Nyasa na Namtumbo ambapo chuo cha VETA Namtumbo kimegharimu Tsh. biln. 4. Na VETA Nyasa Tsh. 2,196,581,105.29 na hivyo ufanya jumla ya fedha iliyotumika kuwa shilingi 6,196,581,105.29
Vyuo vya Ualimu na Elimu ya Juu
Vyuo vya Ualimu
Mkoa una vyuo vya ualimu 3 vinavyotoa mafunzo ya ualimu. Kati ya hivyo chuo cha ualimu Songea ni cha Serikali na 2 ambavyo ni chuo cha ualimu Kiuma na Chuo cha Ualimu Nazaleti vinamilikiwa na mashirika binafsi.
Ili kuweka mazingira bora ya kufundisha na kujifunzia katika kipindi cha miaka mitano Mhe, Rais ametuletea fedha kwa ajili ya ukarabati wa chuo cha ualimu Songea kwa thamani ya fedha shilingi 1,485,760,357.26.
Elimu ya Juu
Mkoa kwa kushirikiana na Serikali, wadau wa maendeleo unaendelea kuhamasisha uwekezaji katika eneo la uanzishaji wa vyuo vya elimu ya juu. Hadi kufikia mwaka 2020 kuna vyuo vya elimu ya juu 3 ukilinganisha na uwepo wa chuo 1 ilipokuwa 2015. Vyuo hivyo ni matawi 2 ya Chuo Kikuu huria cha Tanzania katika wilaya ya Tunduru na Songea. Vyuo vingine ni Tawi la chuo Kiuu Cha Kilimo Sokoine (SUA) kilichopo wilaya ya Tunduru na chuo cha maliasili na Utalii kinachojengwa wilaya ya Nyasa.
Katika utekelezaji wa Ilani ya CCM ya miaka mitano jumla ya miradi 2558 yenye thamani ya shilingi 8,525,829,742 inaendelea kutekelezwa katika ujenzi wa miundombinu ya madarasa, vyoo vya wanafunzi, mabweni na mabwalo kama ilivyoainishwa katika jedwali lifuatalo;
ELIMU YA MSINGI |
||
Madarasa |
128 |
2,560,000,000 |
Matudu ya vyoo |
1107 |
3,966,229,742 |
ELIMU YA SEKONDARI |
||
Madarasa |
38 |
760,000,000 |
Matundu ya vyoo |
36 |
39,600,000 |
Mabweni |
10 |
800,000,000 |
Mabwalo |
4 |
400,000,000 |
JUMLA |
2558 |
8,525,829,742 |
Shughuli nyingine zilizotekelezwa na mafanikio yaliyopatikana kwa mwaka 2015-2020
Mafanikio haya yanayoonekana wazi kwa kipindi cha miaka mitano katika sekta ya elimu yametokana na utashi mkubwa alionao Mhe. Rais katika kuwaletea maendeleo watanzania kupitia sekta ya elimu.
ITAENDELEA KATIKA SEKTA YA AFYA
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.