UZALISHAJI wa mazao mkoani Ruvuma umeongezeka kutoka tani 1,623,509.57 msimu wa mwaka 2020/2021 hadi kufikia tani 1,823,509.57 katika msimu wa mwaka 2022/2023.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesema kuongeza kwa uzalishaji wa mazao hayo kumechangiwa na wakulima kuongeza matumizi ya mbolea ya ruzuku ambayo imeweza kuwafikia wananchi katika maeneo yao kwa gharama nafuu.
Amebainisha kuwa kutokana na serikali kuweka ruzuku kwenye mbolea. matumizi ya Mbolea yameongezeka kutoka tani 50,524.50 msimu wa 2021/2022 hadi tani 93,955.7 msimu wa 2023/2024.
“Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kufanya maboresho makubwa katika Sekta ya Kilimo kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya kilimo, mifumo ya ruzuku ya pembejeo na vyombo vya usafiri kwa Maafisa Ugani’’,alisisitiza Kanali Abbas.
Amesema Serikali imetoa pikipiki 281 kwa maafisa ugani wote wa Kata na Vijiji kwa kwa Mkoa wa Ruvuma kwa lengo la kuwawezesha Maafisa Ugani kuwafikia wakulima ili kutoa huduma za ugani kwa wakulima.
Ameongeza kuwa serikali pia imetoa mashine saba za kupima afya ya udongo na kwamba Mkoa wa Ruvuma kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo kupitia Taasisi yake ya TARI Uyole na Kampuni ya OCP iliwezesha upimaji wa Afya ya Udongo katika vijiji 100 vya Mkoa wa Ruvuma.
Ameongeza kuwa serikali imejenga maghala 31 yenye uwezo wa kuhifadhi tani 1,000 kila moja katika Halmashauri za Madaba ambako yamejengwa maghala 11, Halmashauri ya wilaya ya Songea maghala 12 na Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo yamejengwa maghala manane kupitia program ya ujenzi wa maghala kwenye maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa mazao ya nafaka.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.