Kampuni ya simu ya Vodacom imezindua duka jipya lililoboreshwa katika eneo la Bombambili Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed aliyewakilishwa Afisa Biashara Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Martin Mabaro.
Akizungumza kwenye hafla hiyo mgeni rasmi amewapongeza kampuni ya Vodacom kwa kusogeza huduma muhimu karibu Zaidi na wananchi ambapo amesisitiza kuwa mawasiliano ni chachu ya maendeleo ya kiuchumi.
Amesema huduma za mawasiliano zinachangia kwa kiasi kikubwa kuondokana na umaskini na kukuza biashara ambapo ametoa rai kwa Kampuni nyingine za mawasiliano kuiga mfano wa Vodacom kwa kuwa Mkoa una fursa nyingi za uwekezaji.
“Ruvuma ni Mkoa wa kilimo na biashara,hivyo uwepo wa duka hili utasaidia katika kuwahudumia wakulima na wanunuzi pindi wanapohitaji huduma ndani ya Mkoa wetu hivyo naamini huduma hii itatupa manufaa makubwa’’,alisisitiza.
Katika hatua nyingine mgeni rasmi amepongeza huduma ya m-mama inayotolewa na Vodacom ambayo amesema imekuwa msaada mkubwa kwa akinamama wajawazito na Watoto wachanga pindi wanapopata dharura hivyi kuokoa Maisha yao.
Awali akizungumza kwenye hafla hiyo Mkurugenzi wa Hatari na Uzingatiaji wa Vodacom Agapinus Tax amesema uzinduzi wa duka hilo ni hatua endelevu ya Vodacom katika kuwaweka wateja wake karibu Zaidi.
Amesema Vodacom wanaendelea ,kufungua maduka ya kisasa katika Wilaya ya Songea kwa kuwa wamebaini kuwa Wilaya hiyo ina fursa lukuki za kibiashara kutokana na muingiliano mkubwa baina ya Tanzaniaia ,raia wa nchi Jirani na wafanyabiashara mbalimbali.
Amesema kupitia duka hilo wateja watapata huduma bidhaa mbalimbali ikiwemo simu za kisasa na kwamba duka hilo litachangia uwezeshaji kwa wafanyabiashara na wajasirimali wadogo kutokana na huduma ya M-pawa itakayowasaidia kutunza fedha zao.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.