Wananchi wa vijiji vya Magazini, Sasawala, Amani na Likusanguse wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwapatia gari la kubebea wagonjwa katika Kituo cha Afya cha Magazini, hatua ambayo wamesema itapunguza vifo vinavyotokana na ucheleweshwaji wa huduma za rufaa.
Kituo hicho kiko umbali wa zaidi ya kilomita 230 kutoka makao makuu ya wilaya hiyo ambapo ndipo ilipo hospitali ya Serikali ya Wilaya ya Namtumbo.
Wakizungumza kwenye hafla ya makabidhiano, wananchi walionesha furaha yao mbele ya Mbunge wa Jimbo la Namtumbo, Mheshimiwa Vita Kawawa, ambaye ndiye aliyekabidhi gari hilo.
Chifu wa kabila la Wayao katika eneo la Magazini, Thabiti Shaibu Nnambi, alisema wamepoteza zaidi ya watu kumi kutokana na ukosefu wa gari la wagonjwa.
Alimshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mbunge Kawawa kwa juhudi za kuhakikisha huduma bora zinawafikia wananchi wa maeneo ya mbali kama Magazini.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Dr.Aron Hyela, alieleza kuwa Kituo cha Afya cha Magazini ni miongoni mwa vituo 60 vya huduma za afya wilayani humo na kimepokea zaidi ya Shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa majengo mbalimbali
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Jonah Katanga, alisema serikali imeendelea kuboresha huduma kwa wananchi wa kata hiyo kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.