WAKULIMA wa vijiji vya Magazini,ligunga na lusewa wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wameeleza changamoto ya kuwepo kwa ugonjwa wa kukauka majani ya miti ya mikorosho na kuathiri mapato ya uzalishaji wa zao hilo.
Rashidi Ngunda na Daudi Hamisi wakulima wa Korosho kutoka kijiji cha Magazini walisema kuna ugonjwa ambao unawashangaza wakulima wa korosho wa kukauka majani ya miti ya mikorosho na kusababisha mikorosho kutotoa maua na kuathiri uzalishaji wa zao hilo.
Chande Makale meneja wa chama cha Msingi cha Magazini alidai ugonjwa wa kukauka kwa majani ya mikorosho hupunguza uzalishaji wa zao hilo kutokana na wakati wa mikorosho kutoa maua majani ya mikorosho yanayotegemewa kutoa maua yanakuwa tayari yamisha kauka.
Hata hivyo bwana Makalealidai chama kupitia vikao mbalimbali vilipokea malalamiko ya wakulima kuhusu majani ya mikorosho kukauka na kuliwasilisha jambo hilo kwenye bodi ya chama kikuu cha ushirika TAMCU kilichopo wilaya ya Tunduru.
Makale alidai kodi ya zao la korosho inayokatwa wakati wa mauzo ya zao hilo ifanye hiyo kazi ya kuhudumia mikorosho inayokauka majani bila ya kufahamika tatizo la majani hayo kukauka na kusababisha uzalishaji hafifu.
Wakulima hao pamoja na mambo mengine wameishukuru serikali ya awamu ya sita ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa mbolea ya ruzuku na kuiomba serikali hiyo wawasaidie dawa ya mikorosho katika mfumo wa ruzuku.
Stephen Nchimbi mhariri kutoka jukwaa la wahariri Nchini aliwaambia wakulima hao kuwa swala lao la kukauka kwa majani ya mikorosho litamfikia waziri wa kilimo Hussein Bashe bila wasiwasi wowote kwa kuzungumza naye pamoja na kumrushia mahojiano aliyoyafanya na wakulima hao.
Wilaya ya Namtumbo ina jumla ya kata 21 na kati ya kata hizo ni kata 3 ya Magazini,lusewa na Msisima ndizo zinazolima zao la korosho kwa wingi katika wilaya ya Namtumbo .
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.