MNADA WA UFUTA WAINGIZA SHILINGI BILIONI 2 NAMTUMBO
Namtumbo, 22 Mei, 2019
Wakulima wa ufuta wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wamepongeza serikali kwa usimamizi mzuri wa soko la zao hilo kupitia mnada uliowezesha kulipwa shilingi bilioni mbili .
Akizungumza wakati wa mnada wa pili wa zao la ufuta uliofanyika jana Namtumbo ,mwenyekiti wa chama kikuu cha Ushirika cha Songea na Namtumbo (SONAMCO )Salum Brashi amesema,serikali imefanya uamuzi sahihi kuanzisha minada ya ufuta
“Bei ya ufuta katika mnada wa leo imeweza kupanda kutokana na wanunuzi wengi kujitokeza hapa Namtumbo hivyo kufikia kilo kuuzwa shilingi 3,061 tofauti na mnada wa kwanza kilo iliuzwa shilingi 3,010 “alisema Brashi
Alisema haya ni mafanikio makubwa na ukombozi wa kiuchumi kwa wananchi wa Namtumbo
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mnada wa pili wa ufuta ,Afisa Kilimo Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Enock Ndunguru alisema jumla ya makampuni 13 yalijitokeza kuomba kununua ufuta
Ndunguru alisema kwenye mnada huo jumla ya tani zilizokuwa katika ghala ni 666.26 ambapo bei ya juu iliyofikiwa na kampuni ilikuwa shilingi 3,061
Kampuni ya YIHAI Kerry toka China ilitangazwa kushinda mnada huo kwa kununua tani 400 kwa shilingi 3,061 ikifuatiwa na kampuni ya Export Trading ya Tanzania ikinunua tani 266.2 zilizosalia kwa shilingi 3,050 kwa kilo ya ufuta.
“Jumla ya shilingi 2,034,630,000/- zimepatikana kwenye mnada huo ambapo bei ya uwiano ni shilingi 3,055 huku mkulima akilipwa shilingi 2,774.04 kwa kilo ya ufuta na makato yote yatakuwa shilingi 281 kwa kilo “ alisema Ndunguru
Mnada wa kwanza wa ufuta katika wilaya ya Namtumbo ulifanyika wiki iliyopita ambapo jumla ya tani 240.26 zenye thamani ya shilingi 723,201,263 zilipatikana kwa bei ya shilingi 3,050 kwa kilo.
Kwenye mnada huo wa kwanza kampuni ya Sunshine Commodities Private ltd ya Mtwara ilishinda kati ya kampuni saba zilizojitokeza.
Mwisho
Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Ruvuma.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.