Wafanyabiashara waliokwenda kupinga mfumo wa Stakabadhi Ghalani mahakamani, kwa mazao ya Mbaazi na Soya mkoani Ruvuma, wakimlalamikia Mkuu wa Mkoa Kanali Labani Thomas na Mamlaka za Halmashauri za Wilaya, wameshindwa katika shauri hilo.
Mahakama Kuu Kanda ya Songea imesema miongozo ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kuhusu namna ya uuzaji wa mazao hayo ni halali kwa mujibu wa sheria na Mamlaka ya Mkoa.
Wakulima wa Mkoa wa Ruvuma wanaipongeza serikali kwa kuanzisha Mfumo wa stakabadhi ghalani ambao umekuwa na faida nyingi kwa mkulima na ushirika
Mikoa mingi nchini hivi sasa imeanza kutumia mfumo huo unaoleta tija kutokana na bei nzuri na soko la uhakika kwa mkulima.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.