Wanachama na wapenzi wa Simba wamejitokeza kwa wingi kutoa damu katika hospitali ya Rufaa ya Songea (HOMSO) kwa ajili ya kusaidia wagonjwa waliolazwa Hospitalini hapo .
Wanachama hao wamejitolea damu ikiwa ni wiki ya Kilele cha Simba 2024 ambapo wamekuwa wakichangia damu kila mwaka.
Mwenyekiti wa Matawi yote ya Simba Juma Ndago amesema wamekuwa wakifanya hivyo kila mwaka kwa lengo la kumuomba Mwenyezi Mungu na kurejesha kidogo kwa jamii hasa kwa watu wenye uhitaji.
"wanachama wa Simba wamekuwa na desturi ya kuchangia damu na kujitolea vifaa mbali mbali kwa watu wenye matatizo mbalimbali”,alisema Ndago..
Zedania Mgale ,Kiongozi wa wanachama hao amesema kuchangia damu ni sadaka kubwa kwani wanaenda kusaidia watu wenye shida
Kwa upande wake Mwanachama Ester Nyilenda amesema , Wagonjwa wengi wanashida ya damu na wanahitaji msaada hivyo wananchi ,wasiogope kutoa damu.
Naye ,Yassin Mohammed, amesema wananchi waige ambacho wanasimba wanakifanya kwani raha ya mwanasimba yoyote ni kushinda na kusaidia watu wenye mahitaji.
Said Abdallah Mtumishi kitengo cha Damu salama kinahitaji unit zaidi ya 300 uhitaji na kwamba ,uchangiaji utasaidia kupunguza vifo vya akina mama wajawazito ,watoto na wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji.
Ametoa rai kwa wananchi wajitokeze kuchangia damu ili kuhokoa maisha ya ndugu zetu wenye uhitaji wa Damu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.