Wananchi wa Halmashauri ya Madaba Wilaya ya Songea wameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayongozwa na Mheshimiwa. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea daraja jipya kwani ujenzi wa daraja hilo utasaidia kuepusha Maafa.
Wananchi hao wametoa shukrani hizo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo la mawe katika barabara ya Lipupuma-Mgombezi-Chechengu Halmashauri ya Madaba lililogharimu shilingi milioni 153 badala ya milioni 500.
"Tunaishukuru Serikali kwa kutujengea daraja hili maana kwa sisi wakulima litaturahisishia kusafirisha mazao yetu kwasababu tulikuwa tunapa shida sana watu wengi maeanguka kwasababu ya madaraja ya miti ila kwasasa tumejingewa daraja imara tunaishukuru Serikali kwa kutujengea"
Daraja hilo linaunganisha vijiji vya Lipupuma,Mgombezi na Chechengu ambapo linajengwa na Kampuni ya Gewa General Enterprises ya Morogoro kwa usimamizi wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA)
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.