Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga wametakiwa kutumia fursa zitokanazo na uwepo wa nishati ya makaa ya mawe ili kujinusuru na changamoto za kiafya na za uhifadhi mazingira
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Kisare Makori wakati wa hafla ya ugawaji wa tani 10 za nishati mbadala itokanayo na makaa ya kwa shule za msingi 15 pamoja na sekondari 15 kwa ajili ya kupikia
Makiro ameipongeza Halmashauri hiyo kwa uamuzi wa kutumia nishati safi kwani takwimu zinaonyesha zaidi ya hekta mia tisa za miti sawa na miti milioni moja na elfu thelathini ukatwa kila mwaka kwa matumizi ya kupikia.
Amesema Serikali inaunga mkono sera mbalimbali za kimataifa kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia na uhifadhi mazingira ili kupunguza matumizi ya nishati chafu na isiyo salama katika Nyanja za kijamii, kiuchumi, kiafya na kimazingira
“Niwapongeze kikundi cha Wanawake Mbalawala ambao ni wanufaika wa mkopo wa 10% kwa ubunifu na kutumia fursa zilizopo katika kuunga mkono juhudi za serikali katika matumizi ya nishati mbadala ambayo ni chachu katika kuhifadhi mazingira”amisema DC Makiro
Pia amesema ili biashara ya kukata kuni na matumizi ya mkaa yafike kikomo ni lazima wananchi wabadilike kwa kuacha kukata miti hivyo pia amewataka viongozi wa taasisi na wadau kuendelea na juhudi za upandaji miti na kupinga shughuli za kilimo kwenye vyanzo vya maji
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbinga Joseph Rwiza amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha katika kata zote kupitia viongozi ili wateo elimu ya nishati safi kwa wananchi ikiwemo na sehemu zinazo hudumia watu wengi kama vile mashuleni lengo
“Nimejipanga katika Halmashauri yetu kuhakikisha shule zetu zote za msingi na sekondari tunalisimamia ndani ya muda mfupi kuanza kutumia nishati mbadala ya makaa ya mawe ili kuhakikisha zoezi linakuwa endelevu na kuunga mkono wazalishaji wetu wa nishati safi” amesema Rwiza
Akizungumza kwa niaba ya walimu wakuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mndeme mwalimu Denterias Mgaya amesema mkaa huu utapunguza gharama lakini pia ni chachu katika kutunza mazingira.
Watengenezaji na wauzaji wa mkaa huo ni kikundi cha wanawake Mbalawala kilichopo kata ya Ruanda kikundi ambacho ni wanufaika wa mkopo wa 10% unaotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
|
|
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.