BAADHI ya wananchi wa kijiji cha Utili,kata ya Utili wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma,wameuomba Wakala waMaji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kuwakabidhi mradi wao wa maji ili waweze kuhudumia na kufanya matengenezo ya miundombinu pindi inapoharibika.
Wametoa maombi hayo kwa Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Mbinga Davis Charles,aliyetembelea mradi huo ulioanza kutekelezwa Mei 2022 na kukamilika Januari 2023.
Akizungumza baada ya kutembelea mradi hip Mhandisi David Charles amesema ,mradi wa maji Utili umesanifiwa kuhudumia watu 3,626 na utekelezwa kwa gharama ya Sh.milioni 428,434,692.
Amezitaja kazi zilizopangwa kutekelezwa katika mradi huo ni ujenzi wa tanki la ujazo wa lita 150,000, kujenga chanzo cha maji,uchimbaji wa mitaro na ulazaji wa bomba za kusambaza maji urefu wa kilomita 13.6 na ujenzi wa vituo 14 vya kuchotea maji.
Amesema utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 98 na kazi zilizobaki ni uwekezaji wa mfumo wa kutibu maji na usimikaji wa alama kwenye njia za bomba za maji.
Ameongeza kuwa ,hadi sasa utekelezaji wa mradi huo umekamilika kwa asilimia 100 na upo chini ya uangalizi wa mkandarasi ambao utaishi mwezi ujao na baada ya kipindi hicho utakabidhiwa kwa wananchi.
Ametoa rai kwa wananchi wa kijiji hicho,kuhakikisha wanalinda miundombinu ya mradi huo ili uwe .endelevu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.