WANANCHI wa kijiji cha Mahilo kata ya Kitula Halmashauri ya wilaya Mbinga mkoani Ruvuma,wameiomba Serikali iwasaidie kukamilisha ujenzi wa Zahanati waliyoijenga wao wenyewe ili ianze kutoa huduma na kuwaondolea kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.
Zahanati hiyo inatarajia kuhudumia zaidi ya wakazi 3,000 wa kijiji hicho kati ya wakazi 9,000 wa kata ya Kitula na hadi sasa imegharimu Sh.milioni 45 kati ya hizo Sh.milioni 13 michango ya wananchi wenyewe,Sh.milioni 28 zimetolewa na Halmashauri ya wilaya Mbinga
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema,tangu kijiji hicho kilipoanzishwa hakuna huduma za afya, badala yake wanategemea kupata huduma hizo wilaya jirani ya Nyasa kilometa 20 na Hospitali ya Misheni Litembo iliyopo umbali wa kilometa 15.
Diwani wa Kata ya Kitula Mheshmiwa Alex Ngui,amewapongeza wananchi wa kijiji hicho kwa uamuzi wa kujenga zahanati ambayo itawasaidia kupata huduma za afya uhakika na karibu na maeneo yao.
Hata hivyo,ameungana na wananchi wa kijiji hicho kuiomba Serikali kuharakisha kufungua zahanati hiyo ili wananchi wapate huduma na kuokoa vifo vinavyotokana na kukosa huduma za afya.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.