Mthamini na Mratibu wa kodi ya aridhi Mkoa wa Ruvuma Herbert Mlowe amewataka Wananchi mkoani umo wachangamkie msamaha wa riba kodi ya pango la Aridhi uliotolewa na Rais kuanzia mwezi julai hadi Desemba 2022
Hayo ameyasema katika mkutano na wananchi uliofanyika kata ya Ruhuwiko manisapaa ya Songea mkoani Ruvuma wakati wa zoezi la kukabidhi hati miliki za viwanja kwa wananchi hao baada ya kurasimisha Aridhi zao
Mlowe alisema Serikali imetoa msamaha huo kwa watu ambao wana malimbikizo riba ya kodi ya pango la Aridhi kuanzia mwaka 1996/97 hadi 2018/19 hivyo wamepewa msamaha kwa kuondolewa riba na wanatakiwa kulipa kodi ya msingi tu
“Rais Samia Suluhu Hassani ameridhia kusamehe riba ya kodi ya pango la aridhi kwa wadaiwa sugu kwa masharti kwamba wadahiwa hao wawe wamelipa madeni ya msingi ndani ya mienzi sita kuanzia mwezi Julai hadi Desemba mwaka huu” alisema Mlowe.
Hata hivyo amewapongeza ambao wamekabidhiwa hati zao alisema hatua ya kumilikishwa ardhi kwa nyaraka kuna faida kubwa katika maisha ya kila siku kwani itasaidia kuongeze usalama wa aridhi, kupunguza migogoro na nyaraka hiyo kutumika kama dhamana.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.