WAKAZI wa mitaa mitatu ya Osterbay,Miembeni na Kiswele kata ya Msamala Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma,wameiomba serikali kupitia wakala wa barabara za mijini na vijijini(TARURA)kufanya matengenezo ya barabara zake ili ziweze kupitika kirahisi.
Wamesema,kwa sasa barabara nyingi kwenye maeneo hayo ni mbovu na baadhi ya watu wanalazimika kulipia gharama ya kupaki magari yao kwenye vituo vya mafuta kwa kuwa wanashindwa kufika nayo nyumbani.
Menald Mwanditi mkazi wa mtaa wa Kiswele asema,katika kipmeindi hiki ambacho mvua bado zinaendelea kunyesha kwa wingi, hali inakuwa mbaya zaidi hasa maji yanayotoka barabara kuu ya Songea-Makambako iliyoko chini ya wakala wa barabara Tanzania (TANROADS).
Amesema,katika barabara hiyo kuanzia katikakituo cha mafuta Ottawa hadi Chuo cha Top One Inn maji yanapita juu ya barabara na kuelekea upande wa pili ambako kuna makazi ya watu kwa kuwa yanashindwa kupitia kwenye mifereji ambayo imeziba kutokana na kujaa mchanga na takataka mbalimbali.
Kwa mujibu wa Mwanditi,barabara nyingi za mitaa za TARURA kwa sasa zimeharibika na hazipitiki kwa kuwa hazijafanyiwa ukarabati wowote tangu zilipotengenezwa hivyo kuwa na mashimo makubwa yanayojaa maji na kuhatarisha usalama hasa kwa watoto wadogo.
Mkazi wa Msamala Leonald Kapinga amesema, kukosekana kwa mifereji ya kupitisha maji ya mvua katika barabara kuu ya Songea-Makambako ina sababisha mchanga unaosombwa na maji kujaa kwenye makazi yao na hivyo kuingia gharama kubwa ya kuondoa mchanga huo.
Ameiomba TARURA na TANROADS mkoani Ruvuma,kufanya matengenezo ya barabara zao ili kuwaondolea adha inayowakabili kwani kuna hatari ya kufunga biashara zao kwa kukosa wateja.
Kaimu Meneja wa TARURA wilaya ya Songea Godfey Mngale amesema,kabla ya kilio cha wananchi wa Msamala,tayari serikali kupitia TARURA ilishaanza kuchukua hatua kwa kufanya matengenezo ya barabara katika mitaa hiyo.
Amesema,tatizo lililojitokeza kwa sasa ni Mkandarasi amelazimika kusimamisha kazi kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha,lakini mara mvua zitakapokatika kazi ya matengenezo ya barabara katika maeneo hayo zitaendelea kama kawaida.
Amewatoa hofu wananchi wa Msamala kuhusu ubovu wa barabara na kusisitiza kuwa,serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imejipanga kwa kuhakikisha inaboresha miundombinu ya barabara zote ili kurahisisha usafiri na usafirishaji.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.