MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma pichani kushoto Mheshimiwa Juma Pandu ameiomba Serikali kuona umuhimu wa kuligawa jimbo la Namtumbo ili wananchi waweze kupata huduma mbalimbali kwa urahisi tofauti na hivi sasa jimbo hilo lina kata 21 ambalo kijografia kata zake zimekaa mbali na makao makuu ya halmashauri hiyo ambalo linapakana na Wilaya ya Tunduru,Mkoa wa Morogoro na Nchi jirani ya msumbiji.
Pandu ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mkongo Nakawale amesema kuwa kwa ujumla hali ya wananchi ambao wanahitaji kupata huduma ya halmashauri wamekuwa wakipata usumbufu mkubwa namna ya kufika makao makuu ya Halmashauri .
Amesema kuwa wakazi wa maeneo za Kata za Magazini na Lusewa ambazo zipo umbali wa kilomita Zaidi ya 280 hadi makao makuu ya Wilaya wamekuwa wakishindwa kusafiri au kutekeleza baadhi ya miradi ya maendeleo kwenye kata zao kutokana na umbali uliopo na miundombinu ya barabara hasa kipindi cha masika inakuwa mibovu.
Pandu amesema kutoka kata ya kitanda hadi makao makuu ya wilaya ya namtumbo kuna umbali wa Zaidi ya kilomita 150 jambo ambalo limekuwa likisababisha shughuli mbali mbali za maendeleo kuto tekelezwa kwa wakati kutokana na miundo mbinu ya barabara kuwa mibovu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.