Wanawake wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru wameadhimisha uzinduzi wa Siku ya Wanawake Duniani kwa kutoa misaada mbalimbali kwa wahitaji, wakiongozwa na Mhe. Mariam Nyoka, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma.
Sherehe hizo zilifanyika katika kata ya Nakapanya, wilayani Tunduru.
Katika hafla hiyo, wanawake waliojifungua katika Hospitali ya Wilaya ya Tunduru walikabidhiwa zawadi kama ishara ya kuwapongeza na kuwapa moyo katika safari yao ya uzazi.
Mbali na hao, misaada pia ilitolewa kwa watu wenye mahitaji maalum na watoto yatima.
Lengo la sherehe hizo lilikuwa ni kuonyesha mshikamano wa wanawake wa Tunduru katika kusaidia jamii, pamoja na kuhamasisha wanawake wengine kujitolea na kuchangia maendeleo ya jamii.
Wanawake wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru walitoa shukrani kwa wadau wote waliosaidia kufanikisha sherehe hizo na wakaahidi kuendelea kujitoa kwa jamii.
Maadhimisho haya yalikuwa sehemu ya maandalizi kuelekea Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa tarehe 8 Machi kila mwaka, ikiwa na kauli mbiu: “Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji.”
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.