MKURUGENZI Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed amewaagiza wataalam wa Uvuvi katika Halmashauri hiyo kuanzisha shamba darasa la mabwawa ya samaki kwa kila kata.
Hayo amesema katika kikao cha Lishe cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2023/2024 kuwa mara baada kufanikiwa kuanzisha kilimo cha mboga mboga katika shule, waanzishe ufugaji wa samaki ili kusaidia ulaji wa samaki kwa wanafunzi na wananchi.
“ sisi tumesaini mikataba ya lishe nitoe fursa hii kuendelea kutekeleza mkataba wa Lishe ili tuweze kufika malengo ambayo ni asilimia 100”.
Aidha ametoa rai katika idara hiyo kuanzisha mnada wa kuku ili kuhamasisha ufugaji wa kuku kwa wananchi na shule ambao utasaidia ulaji wa mayai na nyama na kuongeza mapato kwa wananchi na Halmashauri kwa ujumla
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.