Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, Bi. Elizabeth Gumbo akiambatana timu ya Menejimenti ya Halmashaui ya Wilaya ya Songea, wametembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayosimamiwa na Halmashauri na kutoa maelekezo na maagizo kwa mafundi na kamati ya ujenzi kuhakikisha wanakamilisha miradi hiyo kwa wakati.
Katika ziara hiyo timu ya menegiment ilikagua Miradi ya Afya ambayo ni zahanati vituo vya Afya, Shule za Msingi na Sekondari. Miongoni mwa shule hizo ni pamoja na Shule ya Msingi Nambalapi, Mbolongo Shule ya Sekondari Jenista Mhagama, Shule ya Sekondari ya Mpitimbi na Soko la Mazao la Kimkakati lililopo kijiji cha Matomondo, mradi wa mabwawa ya Samaki uliopo Mpitimbi
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.