WATOTO wa Walengwa wa TASAF wanaomaliza kidato cha Tano na kuingia Chuo kikuu wapewa kipaumbele cha Mkopo wa asilimia 100.
Hayo amesema Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama katika Halmashauri ya Madaba Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma.
Mhagama amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed kuhakikisha watoto wanaotoka katika kaya Masikini na kunufaika na Mradi wa TASAF wanaomaliza kidato cha Sita na kuingia chuo kikuu kupata asilimia 100 ya Mkopo pamoja na wale wanaomaliza darasa la Saba na kidato cha nne wanaofeli wahakikishe wanajiunga na Elimu ya Veta.
“Watoto wa Walengwa wa TASAF wanaomaliza kidato cha tano na kujiunga na chuo kikuu wapewe mkopo asilimia 100 na wanaomaliza Darasa la Saba na kidato cha nne wanaofeli wajiunge na VETA na Serikali itawalipia”.
Mhagama ametoa rai kwa viongozi wa Halmashauri ya Madaba kuhakikisha walengwa wanaohama ruzuku ziwafikie popote walipo isipokuwa kwa wale walioaga dunia wasitishiwe.
Hata hivyo amesema tathimini ifanyiki ikiwa kwa wale ambao wamekwisha fika katika hali nzuri wasitishiwe mradi huo wapewe wengine wanaoishi katika kaya maskini.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas amempongeza Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwajali wananchi maskini kwa kuwapatia ruzuku ya TASAF.
“Nilipokuwa nawaangalia wazee wangu nimekumbuka nyumbani na tumepata fursa ya kuzitembelea nyumba mbili wametoa shukrani jinsi gani Rais anavyoendelea kuwajali wananchi maskini”.
Mtendaji wa Kijiji cha Mtyangimbole Joseph Ngatunga amesema mafanikio ya mpango wa kunusuru kaya maskini katika kijiji hicho walengwa pamoja na wananchi kwa ujumla wanaonufaika na ruzuku imesaidia kuboresha makazi,mavazi pamoja na chakula.
Amesema walengwa wamefanikiwa kuongeza kipato katika kaya kupitia ujira waliopata kutokana na ushiriki wao wa kazi,kuongezeka idadi ya watoto wanaohudhulia shule,Afya za Watoto zimeimalika kwa kuhudhulia kliniki.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Agosti 16,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.