KANISA la Anglikani linaloshilikiana na Shirika la Copassion wamegawa Magodoro 100 kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu yenye thamani ya shilingi milioni kumi.
Akitoa taarifa hiyo leo baada ya ibada ya Shukrani ya watoto hao Afisa utawi wa mtoto Fidea Mapunda kwa aliyekuwa mgeni rasmi baada ya Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeti Mgema Diwani wa Kata ya Subira kabla ya kugawa Magodoro amesema vituo hivyo vya kulelea watoto wanaishi katika mazingira magumu vilianza Januari 2020.
“Changamoto ni kubwa kwa sasa ni kutokuwa na miundombinu ya choo kwani tuna tundu moja tu,Ombi letu kwako kutuombea kwa Mungu afungue njia ya kufanikisha usalama wa watoto wetu”.
Mapunda amesema Magodoro yatayotolewa kwa awamu mbili ikiwa mpaka kufikia sasa kituo cha Mjimwema kina watoto 150 na watoto hamsini wemepatiwa na kituo cha Lupapila wamepokea watoto hamsini na waliobaki watapatiwa kwa kipindi kijacho.
Kwa upande wake Mgeni rasmi Diwani wa Kata ya Subira John Ngonyani amelishukuru kanisa la Anglini kwa kuonyesha upendo kwa kata ya Subira na kuwekeza katika Elimu kwa watoto wenye Mazingira Magumu.
Diwani baada ya hotuba yake amechangia shilingi laki moja kwaajili ya Ujenzi wa vyoo na kuwaahidi kusimamia wanapata kivuko,Umeme na Maji katika kata hiyo.
“Mimi kama Diwani najua mmeanza katika mazingira magumu sana Kivuko hakuna,Umeme,Maji ninakazi kubwa sana kuhakikisha miundombinu inakuwa ya uhakika Lupapila Tanescol nimefuatilia kunabajeti wameandaa kufikia 2021 juni umeme utakuwa tayari”.
Hata hivyo Diwani amesema atahakikisha anapambana kuhakikisha anaunga mkono huu mradi wa kusaidia watoto wanaishi katika mazingira magumu ili baadae waweze kufanya vizuri na kuondokana na umaskini.
Naye Diwani wa Kata ya Mjimwema Silvester Mhagama baada ya ibada ya Sikuku ya Chrismas amegawa magodoro kwa watoto 50 wa kituo cha Mjimwema ameahidi kutoa elfu hamsini kwaajili ya mahitaji ya watoto hao na kilo ishirini na tanao za mchele kwa watoto kila mwezi.
Padri John Midelo wa Kanisa la Mjimwema baada ya ibada ya shukra ya kuwawezesha kumaliza mwaka na kuwaepusha na Gonjwa la Corona,kuanzia kufunguliwa kwa vituo hivyo Januari 2020 amesema vituo hivyo vinawatoto kuanzia miaka 3 mpaka 7 na watalelewa mpaka kufikia miaka ishirini na mbili kimwili,kiroho na Kielimu.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa habari Halmashauri ya Madaba
Desemba 25,2020
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.