WATAALAM 50 waliopo chini ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma wameanza mafunzo ya mfumo mpya wa ununuzi wa umma (NeST).
Mafunzo hayo yameanza Agosti 11,2023 kwenye ukumbi wa Mipango Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mjini Songea yakishirikisha watumishi kutoka Sektretarieti ya Mkoa wa Ruvuma na makatibu Tawala wa wilaya zote tano za Mkoa wa Ruvuma ambazo ni Songea,Namtumbo,Tunduru,Mbinga na Nyasa.
Mafunzo hayo yametolewa baada ya timu ya watumishi sita kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Ruvuma kupata mafunzo ya mfumo moya wa Ununuzi NeST yaliandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi ya Umma (PPRA) mjini Dodoma na kushirikisha Sektretarieti za mikoa 26 ya Tanzania Bara.
PPRA imeunda mfumo mpya wa ununuzi wa umma unaoitwa National eprocurement Sytem of Tanzania (NeST) ambao umeanza kutumika Julai Mosi 2023,baada ya kubaini changamoto za kiufundi zilizojitokeza kwenye mfumo wa ununuzi wa awali (TANePS) ambapo Mfumo wa TANePS utakoma rasmi kutumika ifikapo tarehe 30 Septemba 2023,
Faida za mfumo mpya wa ununuzi wa umma kuwa ni Pamoja na kuongeza wigo wa ushiriki kwenye ununuzi,uwajibikaji,kupunguza muda wa mchakato,upatikanaji wa taarifa na kupunguza mianya ya rushwa.
Faida nyingine ni uandaaji wa zabuni zote na uombaji wa zabuni utafanyika ndani ya mfumo,wazabuni watajisajiri na kupandisha nyaraka zao zote kwa mara moja na nyaraka zote zitasainiwa ndani ya mfumo.
Sekta ya ununuzi wa umma inachukua takriban asilimia 70 ya Bajeti ya Serikali hivyo uamuzi wa serikali kuamua kuanza kutumia mfumo wa NeST kutaongeza uwajibikaji kwa watendaji hasa PPRA wanaosimamia mfumo wa ununuzi wa umma.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.