Katibu Tawala Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Mtela Mwampamba amewahimiza wazazi na walezi kuwapa watoto vyakula vyenye mchangonyiko wa mlo kamili.
Mtela ameyasema hayo katika kijiji cha Mtepa Kata ya Lituta Halmashauri ya Madaba wakati wa zoezi la Utoaji wa vifaa mbali mbali vyenye thamani ya shilingi milioni 39 vilivyotolewa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika Shamba la miti Wino Madaba,
Mwampamba amesema licha ya wakazi wa Madaba kuwa na utajiri wa fedha wana changamoto ya kutozingatia mlo kamili ili kuepukana na udumavu kwa watoto chini ya miaka mitano.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Mhifadhi Mkuu wa shamba la miti Wino Groly kasmir amesema kuwa wametoa vifaa hivyo kwa shule za msingi,makanisa,na hospitali kwa lengo la kurejesha sehemu ya mapato kwa jamii .
Amesema wakazi hao wamekuwa Mstari wa mbele kusimamia hifadhi hiyo huku akiwataka kuendelea kuwa walinzi kwa watu ambao wamekua wakitorosha moto unaosababisha hasara kwa serikali na watu binafsi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.