Baraza huru la wazee wa Jimbo la Madaba, likiongozwa na Chief Yukundusi Chabruma Tawete, limemuomba Mbunge wa jimbo hilo, Mhe. Dkt. Joseph Kizito Mhagama, kugombea tena katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ili aendelee kuwatumikia wananchi.
Tamko hilo limetolewa baada ya mkutano wa wazee hao uliofanyika katika Kijiji cha Kipingo, Kata ya Lituta, ambapo walieleza kuridhishwa na kazi kubwa iliyofanywa na mbunge huyo katika kuwaletea maendeleo.
“Tumekaa kama wazee, tumejadiliana na kutambua mchango wako katika jimbo hili. Ni lazima ugombee tena,” alisema mmoja wa wazee waliohudhuria kikao hicho.
Mwenyekiti wa Baraza hilo katika Kata ya Lituta, Bw. Octa Mbilinyi, alisema kuwa wamefikia hatua ya kumuomba mbunge huyo kurejea kugombea kutokana na maendeleo makubwa aliyoyaleta.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Madaba, Mheshimiwa Teofanes Tadei Mlelwa, aliunga mkono ombi hilo, akisema kuwa maendeleo yanayoonekana katika jimbo hilo ni kielelezo cha uongozi mzuri wa Mhagama, hivyo anastahili kuendelea kwa muhula mwingine.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.