Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama, amewasihi waumini wa Kanisa la Kigango cha Liula, Parokia ya Matimira, Peramiho mkoani Ruvuma, kuchangamkia fursa ya upimaji afya bure inayotolewa na madaktari bingwa waliopo mkoani humo, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Pasaka.
Akizungumza , mara baada ya ibada ya Pasaka, Waziri Mhagama amesema kuwa huduma hizo muhimu, hususan za uchunguzi wa magonjwa ya saratani, zinatolewa katika Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Joseph Peramiho na zinahusisha madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), bila gharama kwa wananchi.
“Ninawaomba sana wananchi wa Peramiho na maeneo jirani,Tumieni fursa hii adhimu ya Pasaka kupima afya zenu. Hii ni zawadi kutoka kwa Rais wetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa wananchi wa pembezoni,” amesema Mhagama.
Ameongeza kuwa Serikali inatarajia kuleta pia madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wenye matatizo hayo, ikiwa ni sehemu ya mpango wa Serikali kusogeza huduma za afya karibu na wananchi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.