Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa leo Januari 6, 2023 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Mkoa wa Ruvuma iliyosajiriwa kwa jina la Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyopo wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.
Mradi huo unatekelezwa kwa awamu mbili kwa gharama ya shilingi bilioni 4 kupitia Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP), awamu ya kwanza ilianza April 2022 na inaotarajiwa kukamilika Januari 30, 2023 ambayo itagharimu shilingi bilioni tatu. Shule hiyo itakapokamilila itapokea wanafunzi 1,080 ambapo awamu ya kwanza itapokea wanafunzi 600.
Awamu ya kwanza imehusisha ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo mabweni matano, bwalo, vyumba 12 vya madarasa, jengo la utawala, nyumba ya mwalimu, mfumo wa maji safi na maji taka, vyoo matundu 16, uzio, kichomea taka, chumba cha jenereta na njia za kutembelea.
Aidha, awamu ya pili ambayo ujenzi wake unatarajiwa kuanza ndani ya mwaka huu kwa gharama ya shilingi bilioni moja itahusisha ujenzi wa madarasa 10 yenye ofisi za walimu tatu, chumba cha ICT, Maktaba, nyumba nne za walimu na mabweni manne.
Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwaRais Mheshimiwa Dkt. Samia ameamua kuwekeza kwenye elimu ya mtoto wa kike kwa kujenga shule za wasichana nchi nzima ili kumpunguzia changamoto zilizokuwa zikimkabili. “Si kwamba amemtenga mtoto wa kiume hapana, ameamua kwenda nao wote.”
Pia, Waziri Mkuu amewataka wakandarasi wanaojenga shule hiyo kuhakikisha wanakamilisha ujenzi huo kwa muda uliopangwa ili waanze kupokea wanafunzi. Shule ya Sekondari Dkt. Samia Suluhu Hassan inatarajia kuanza kupokea wanafunzi wa kidato cha tano Julai, 2023.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.