Waziri wa Maliasilii na Utalii Dkt Damas Ndumbaro amezindua mashine ya kisasa ya kuchakata magogo itakayosaida kuongeza thamani ya mnyororo wa mazao ya misitu na uvunaji wenye tija.
Dkt Ndumbaro amefanya uzinduzi huo katika viwanja vya parokia ya Bombambili Manispaa ya Songea
Dkt Ndumbaro amezindua mashine yenyethamani ya shilingi milioni 110 yenye uwezo wa kuchakata mbao 450 kwa siku ambapo itafanyakazi katika Vijiji tisa vilivyofanyiwa upembuzi yakinifu wa matumizi bora ya ardhi na vyenye misitu ya kutosha kupitia mradi wa FORVAC katika Halmashauri ya Wilaya yaSongea na Namtumbo.
Dkt Ndumbaro amesema uwepo wa mashine hiyo unafaida kubwa katika kuongeza thamani ya uchakataji wa mazao ya misitu kwakuwa asilimia 60 ya mazao yanayochakatwa nibidha inayohitajika sokoni tofauti na awali upotefu wa mazao ya misitu ulioneka kuwa mkubwa.
Ametoa rai kwa viongozi wa Taasisi na wadau wa mazao ya misitu kuimarisha uchumi wa wananchi kwakununua na kutumia mazao ya misitu yanayochakatwa na Vijiji kupitia mradi wa FORVAC.
“Uvunaji wa misitu lazima ufanyike bila uvunaji hakuna thamani kwenye misutu”,amesema Dkt Ndumbaro.
Dkt Ndumbaro amewataka wadau wa misitu Nchini wazingatie taratibu na sheria zilizowekwa katika uvunaji endelevu wa misitu pamoja na ulipaji kodi stahiki kwa Taifa,Halmashauri na vijiji wanapochakata mazao ya misitu.
Amewakumbusha wananchi juu ya umuhimu wa kutunza misitu hasa mistu ya asili kwa kutochoma moto ovyo na kuacha shughuli nyingine za kibinadamu ambazo zinasababisha uharibu wa mazngira, mazingira yakiharibiwa yanaathari kubwa kwa viumbehai.
Kwaupande wake mwekiti wa kamati ya maliasili kutoka kijiji cha Muhukuru Lilahi amesema kupitia mashine ambayo Waziri Dkt Ndumbaro ameizindua wanatarajia kuingiza kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 200 kwa mwakajambo linaloonekana kuwa mkombozi wa maisha yao
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.