Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa innocent Bashungwa amelazimika kutumia boti za kienyeji na pikipiki kufika maeneo magumu kufikika katika kijiji cha Mitomoni wilayani Nyasa mkoani Ruvuma.
Waziri Bashungwa alivuka kwa boti Mto Ruvuma kutoka kijiji cha Mkenda Wilaya ya Songea kisha kutumia pikipiki na kufika katika kijiji cha Mitomoni wilayani Nyasa
Baada ya kukagua maeneo hayo, Waziri Bashungwa ametoa miezi miwili kwa Wakala wa Barabara (TANROADS) kufanya usanifu wa kina na upembuzi yakinifu wa ujenzi wa daraja la zege katika eneo la Mitomoni ili wananchi wa maeneo hayo waondokane na adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma mbalimbali za kijamii.
Ujenzi wa daraja hilo utaunganishwa na barabara za Unyoni Mpapa - Liparamba Wilaya ya Nyasa na kijiji cha Mkenda Wilaya ya Songea pamoja.
Kukamilika kwa ujenzi wa Daraja la Mitomoni kutaunganisha Wilaya za Nyasa na Songea mkoani Ruvuma.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.