KAULI Mbiu ya Mwenge maalumu wa Uhuru mwaka 2021 imesisitiza matumizi ya Tehama ni Msingi wa Taifa kwa Maendeleoo Endelevu itumie kwa usahihi na uwajibikaji .
katika kuunga mkono kauli mbiu hiyo Wilaya ya Nyasa imejidhatiti kwa vitendo kwa kuzindua miradi miwili ya Mfumo wa kielekroniki kwaajili ya usimamizi wa matibabu pamoja na matumizi ya mfumo kurahisisha kwa wanafunzi wa shule Ya Sekondari Mbambabay kujisomea kwa urahisi.
Akizungumza kabla ya kuzindua mfumo huo Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Nyasa Jimson Mhagama amesema mfumo huo wa kielektroniki ulianza kutumika Februari 2021 na katika kipindi hicho cha miezi mitano mfumo umeleta mafanikio makubwa.
Mhagama ameeleza Faida za mfumo huo ikiwemo kuongeza uhifadhi na upatikanaji wa taarifa za kitabibu kwa haraka pamoja na Uthibiti na Ukusanyaji wa Mapato, dawa na utunzaji takwimu zote za kitabibu.
“ Fedha zilizotumika katika kufanikisha ufunguzi wa mfumo huo kiasi cha zaidi milioni 33,fedha kutoka Selikali kuu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 21 na Halmashauri shilingi milioni 4.5 pamoja na wahisani kiasi cha shilingi milioni 7.5”
Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa ameelezea jitihada za kuongeza ufaulu katika shule ya Sekondari Mbamba bay imepata ufadhili kutoka Shirika la African child development zikiwemo shule za Sekondari 10 zimepatiwa msaada huo.
Hata hivyo Mhagama amesema mradi huo umegharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 23 ambapo komputa 5 zilitolewa na USCAF zenye thamani ya shilingi Milioni 7.5 na komputa 5 zilitolewa na Tanzania Project zenye thamani ya shilingi milioni 7.5,mtandao wa Internet na vishikwambi 3 vilitolewa na African Child Development zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 3 na ukarabati wa chumba cha komputa zaidi ya milioni 5.
Mhagama ameelezea faida ya kuwepo kwa chumba hicho cha komputa na vifaa kumekuwepo na mafanikio chanya ambayo Halmashauri inajivunia imeweka mkakati wa kusambaza teknolojia.
Upatikanaji wa vitabu kwa urahisi akida na ziada,maswali kwaajili ya mazoezi machapisho na mitihani ya kitaifa iliyopita,kuongeza ari ya kujisomea na ubunifu kwa walimu na wanafunzi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Uhuru Kitaifa amesisitiza matumizi sahihi ya Tehama kwaajili ya kuleta maendeleo Nchini badala ya kutumia kwa kufanya uhali na kupelekea nchi kuingia kwenye machafuko.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Habari ya Mkoa wa Ruvuma
Septemba 5,2021
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.