Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mh. Isabela Chilumba amewataka Wataalamu na Viongozi kuanzia ngazi ya Vijiji, Kata na Halmashauri kusimamia zoezi la utambuzi wa kaya mpya za wanufaika wa TASAF kipindi cha pili ili kupata wanufaika wanaostahili.
Ameyasema hayo jana Tarehe 19 Aprili, 2021 katika Ukumbi wa Kapten. John Komba wakati akifungua Kikao kazi cha kujenga uelewa kuhusu Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Kipindi cha Pili kwa Viongozi, Watendaji na Wawezeshaji katika Ukumbi wa Kapten John Komba Mbamba bay Wilayani hapa.
Chilumba amefafanua kuwa madiwani ni viongozi ambao wako karibu na wananchi, hivyo amewataka mafunzo wanayopewa wakayatumie kushirikiana na wawezeshaji ili kupata wanufaika wanaostahili na kuacha siasa katika zoezi la uibuaji walengwa hao.
Ameongeza kuwa Mpango wa kunusuru kaya maskini kipindi cha pili kinawataka viongozi hao kuwa waaminifu na waadilifu, ili kuondokana na malalamiko ya wananchi ambao watakuwa wanalalamika endapo watachukuliwa wasio na sifa na kuachwa wenye sifa.
Ametoa wito kwa Wataalamu na Viongozi hao kusikiliza mafunzo kutoka kwa wawezeshaji ambayo yatawajengea uwezo wa kutekeleza vema majukumu katika maeneo yao.
Wilaya ya Nyasa imefanya kikao kazi cha kujenga uelewa kuhusu Mpango wa kunusuru kaya maskini Kipindi cha pili kwa Kamati ya Ulinzi na usalama wilaya ya Nyasa, Madiwani, Wakuu wa Idara na Vitengo na Watendaji na Wawezeshaji.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.