WILAYA ya Nyasa ikiendelea na zoezi la Sensa ya watu na Makazi mwitikio kwa wananchi umekuwa Mkubwa .
Mkuu wa Wilaya ya Mbinga amekaimu Wilaya hiyo amesema kuwa zoezi la Sensa katika Wilaya hiyo wananchi wamekuwa na utayari katika kuhesabiwa pamoja na viongozi wa vijiji wametoa ushirikiano katika kuwaongoza Makarani.
Amesema Wilaya ya Nyasa hakuna changamoto ikiwa sehemu maalumu kama Nyumba za Kulala wageni,Hospitali pamoja na Mahabusu Makarani wamepita na zoezi linaenda vizuri.
“Mimi Mkuu wa Wilaya nimehesabiwa Mbinga tangia alfajili natoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano ili Serikali iweze kupanga mipango ya maendeleo”.
Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya amesema amekuwa wakwanza kuhesabiwa kijijini kwake Kihagara asubuhi sana.
Amesema wananchi wananendelea kuhesabiwa hivyo amewapongeza viongozi wote wa Serikali waliofanikisha zoeza hilo akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hata hivyo kupitia zoezi hilo la Sensa amesema kuwa swala la Utalii unaopatikana katika Wilaya hiyo amewakaribisha wawekezaji kuwekeza katika Fukwe ya Nyenda inayopatikana katika Kijiji cha Ndengere Kata ya Mbambabei .
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Agosti 23,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.